IQNA

Qur'ani Tukufu

Mtafiti achunguza nafasi ya 'hamu ya yaliyopita'  katika qiraa ya Qur'ani

18:30 - November 30, 2024
Habari ID: 3479826
IQNA - Visomo vya kale vya Qur'ani Tukufu vinaweza kuwa muhimu kuwasilisha ujumbe aya za Mwenyezi Mungu, mtafiti mmoja amebaini.

Hussein Ghorbani, mtafiti wa qiraa za Qur'ani, aliwasilisha mada yake yenye kichwa cha maneneo kisemacho "Kuchunguza Vipengele Vya Kudumu vya Qiraa ya Qur'ani,"  katika siku ya pili ya Mkutano Maalumu wa 19 wa Wanazuoni Mashuhuri wa Qur'ani, Wasomaji na Wahifadhi, ulioandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa. Baraza Kuu la Quran mjini Tehran.

Ghorbani alianza siku ya Alhamisi kwa kueleza maana ya 'Nostalgia' istilahi ya Kiingereza ambayo pia inatumika katika Kiajemi na kusema Nostalgia kimsingi ni hamu inayotokana na kukumbuka kwa wema mambo ya  zamani.

Kwa mfano, Ghorbani alisema, "Tunaweza kuwa tumekula chakula miongo miwili au mitatu iliyopita ambacho bado tunakitumia hadi leo, lakini mara nyingi tunajiambia au tunawaambia wengine kwamba ladha wakati huo ilikuwa tofauti na nzuri na bado imebakia katika kumbukumbu zetu."

Alibainisha kuwa hisia hii inaweza pia kutumika qiraa ya Qur'ani ya miaka iliyopita. Au wengine hukumbuka walivyokuwa wakisikiliza usomaji maalumu wa ile dua ya daku katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani "Huu ni mfano wa wazi wa kutamani yaliyopita katika ulimwengu wa Quran na dua," aliongeza.

Ghorbani alibainisha sifa kuu za usomaji wa Qur'ani ambayo qiraa yake haisahauliki hata baada ya miongo kadhaa, ikiwa ni pamoja na uzingatiaji kikamilifu vipengele vya kiufundi, mvuto wa qiraa, qiraa ya aina yake, kueleweka, na umashuhuri.

Amesema pia kuna kumbukumbu za qiraa ya kale  kama vile baadhi ya qiraa zilivyomashuhuri kutokana na  uchangamfu wa hadhirina na pia kuna zile qiraa za Maimamu wa Makka na Madina, ambazo hubakia katika kumbukumbu zetu hasa wakati tunaopitazama Al-Kaaba au Msikiti wa Mtume.

Ghorbani alisisitiza, "Katika nostalgia ya maongezi, tunaweza kunukuu visomo maarufu vya Abdul Basit, hasa surah zake fupi, ambazo zimeacha hisia ya kudumu. Kategoria hii pia inajumuisha qiraa zingine mashuhuri kama zile za Saeed Moselm."

Alidokeza kwamba kwa wapenda Qur'ani, nostalgia maalum ina maana kubwa. "Tunachokiona kuwa vipande vya qiraa ya Mustafa Ismail vinaweza visivutie umma wote kwa ujumla, lakini kuna kumbukumbu ya kawaida ya kihisia ambayo hutubadilisha mara tunapoisikiliza qiraa hiyo hata kabla ya kutafakari maana ya aya."

"Kwa kutumia hiyo kumbukumbu ya mema yaliyojiri zamani au nostalgia katika qiraa tunaweza kusikiliza mara kwa mara na kushawishiwa katika kuwasilisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa ufanisi. Tunapaswa pia kulenga kuunda nostalgia mpya katika uwanja wa qiraa kama urithi kwa vizazi vijavyo."

4251061

Kishikizo: qiraa ya qurani
captcha